KWANINI USOME KITABU HIKI
Binadamu wote tunahitaji kujua maarifa ya fedha. Nafahamu kabla ya kugunduliwa fedha, maarifa haya hayakuwa muhimu kama leo. Kipindi hicho, jambo muhimu ilikuwa ni uzalishaji. Unavyozalisha bidhaa nyingi zenye dhamani unakuwa na uwezo mkubwa wa kubadilishana bidhaa mbali mbali na watu wengine. Mfumo huu uliitwa Bata Tredi (Barter trade system).
Maarifa ya fedha na namna ya kuzikamata kwa karne hii hayaepukiki kwa sababu nyingi.
Mwenye maarifa haya anauwezo mkubwa wa kujua namna ya kutengeneza fedha zaidi, kujua namna ya kuzihimili gharama na kuziepuka pale inapostahili, anajua mikopo salama na namna ya kuangalia vigezo vya ukopaji, anajua kuweka kumbukumbu zake vizuri, anafahamu kuandaa bajeti yake n.k. Kupata maarifa ya mambo haya, kunasaidia watu kutatua changamoto mbalimbali za kijamii, kisiasa, kiuchumi, kiroho na kiutamaduni.
Nimekaa karibu na wavuvi nakujifunza mengi. Nimefika kipindi nikaona kukamata Samaki ni kama kutafuta fedha. Fedha ni kama Samaki. Fedha inateleza kama samaki, pia fedha inayeyuka kama barafu. Hizi ni baadhi ya tabia za fedha.