Katika masaa matatu [3] tu ya mwanzo yani hadi kufikia saa 5 usiku idadi ya watu waliopakua Jarida hili walifika 1720 huku waliotembelea kurasa mbalimbali za IDEAS wakifikia 12,000+, Hii inaonesha ni kwa namna gani jarida la IDEAS lilivyo na Content bora kila wiki.
Katika jarida la IDEAS Mada iliyoteka zaidi akili na mioyo ya watu kutokana na komenti zao kwenye mitandao mbalimbali ni mada ya Mahusiano, Katika kipengele hiki jarida la IDEAS limeelezea Mambo mengi ya kupunguza ili kuimarisha mahusiano yako, Ni wakati wako sasa kusoma toleo la kwanza la IDEAS wiki hii na usikose kwani Jarida hili litakujia kila wiki siku ya Jumatani, Hivyo hakikisha hukosi nakala yako.