KWANINI USOME KITABU HIKI
Vijana hupita kwenye matetemeko mbalimbali kipindi cha makuzi yao. Matetemeko hayo unaweza kuyaweka katika makundi ya kiuchumi, kibaolojia, kiimani na kiteknolojia.
Matetemeko haya yanaweza kumfanya kijana asifikie malengo yake. Anaweza kujikuta ameharibu maisha yake bila kupenda. Mtunzi ametoa mifano halisi ya changamoto za tetemeko la ujana alizopitia na jinsi alivyozikabili na kuzishinda. Ametumia mifano ya watu wengine ili kumpa kijana darasa la kutosha anaposoma kitabu hiki. Sote tunajua majuto ni mjukuu, kijana atakayesoma kitabu hiki, ataepukana na mjukuu huyu (Majuto).
Mwisho, mwandishi ametoa mwongozo kwa vijana wanaopenda kuwa wajasiriamali, kujiajiri au kuajiriwa. Mwongozo wa vijana wanaopenda kuwa viongozi katika nyanja mbalimbali pia umetolewa.
Kwa kufanya hivyo, kitabu hiki, kitamsaidia kijana kuyamudu maisha yake ya baadae na hivyo kuwa msaada kwa wazazi, jamii na taifa. Aidha, kitabu hiki kinamfanya kijana asiwe tegemezi. Tuwasaidie vijana kupata nakala ya kitabu hiki. Unaweza kuwapatia kama zawadi. Kwenye ulimwengu huu wa utandawazi mkubwa, maudhui ya kitabu hiki yatawasaidia wazazi kufikia malengo wanayokusudia kwa vijana wao.
Kitasaidia viongozi wa dini kuhimiza kile wanachopenda kukiona kwa vijana. Kitawasaidia viongozi wa vyama vya siasa na serikali, kuona vijana wanafuata misingi ya sheria na taratibu zilizopo na hivyo kuwa viongozi bora. Kwa ufupi, kitasaidia kupunguza vitendo vya uhalifu.
Ni kitabu kinachowafanya vijana wachangie nguvu, akili na maarifa yao katika kujenga uchumi wao binafsi na wa taifa lao. Ni kitabu sahihi kwa kijana mwenye ndoto kubwa!
Nakutakia mafanikio,
Ni mimi mtumishi wako, Peter Mkufya
Mkufunzi na Mhamasishaji Maendeleo
Whatsaap +255 628 673 976