UTANGULIZI KUHUSU KITABU HIKI
Zawadi kwa Watanzania! Tarehe 9-10-2013 nilipewa wazo la kuandika Kitabu hiki. Kazi ya uandishi wa kitabu hiki haikuwa nyepesi. Ilihitaji muda, akili na fedha. Tarehe 25-09-2016 kuanzia saa tatu na nusu asubuhi hadi saa nane na dakika hamsini na mbili mchana (9:30am – 2:52pm), nilikuwa kwenye utulivu mkubwa, nikapokea Kanuni ya Maendeleo ya K.W.E.L.I. Hapo ndipo kazi ya uandishi wa kitabu hiki ilipoanza. Namshukuru Mungu kwa kunipa wazo la kutunga kitabu hiki.
Nitamhimidi Bwana aliyenipa shauri...Zab 16:7a.
Namshukuru mke na watoto wangu kwa msaada walionipa na kwa kunivumilia kipindi chote cha uandishi, kwani ni wazi walikosa kusikia sauti yangu pale nilipokuwa nimetumia muda wao ili kufanikisha kazi hii.

Nakushukuru wewe msomaji kwa maamuzi yako ya kujipatia nakala ya kitabu hiki, kwani kwa kufanya hivyo utajipatia maarifa ya pekee, hivyo kushiriki katika maendeleo yako binafsi na jamii inayokuzunguka. Nimesukumwa kuandika kitabu hiki kwa kutumia elimu na uzoefu wangu ili kuleta kitu kipya kwa msomaji katika maisha ya kila siku, kwa lengo la kukuletea vichocheo vya Maendeleo ikiwa ni pamoja na kupambana na umasikini wa kipato na kifikra.
Mtaalamu mmoja alisema "kila ukuta ni mlango". Kwenye ugumu ndio kwenye fursa.
Unapoendelea kusoma Kitabu hiki utagundua una uwezo mkubwa wakutatua changamoto zako wewe mwenyewe kwanza kabla ya kuhitaji Msaada kutoka mbali. Ikiwa kila Mtanzania atasoma kitabu hiki na kuyafanyia kazi mawazo ya kiuchumi na kijamii yaliyoelezwa, mafanikio yatakuwa dhahiri. Maudhui yaliyo andikwa yataboresha fikra na maisha ya mtu mmoja mmoja, jamii na Tanzania kwa ujumla. Kwa kufanya hivyo lengo la kitabu hiki litakuwa limefikiwa.
Zawadi kwa Watanzania!
Lugha ya Kiswahili imetumika ili kumuwezesha kila mtanzania kusoma na kufaidi mawazo yaliyomo. Yawezekana kwa baadhi ya Watanzania elimu iliyomo humu ikawa ya kawaida kwao, matumaini yangu ni kuwa Watanzania wengi wanahitaji nyenzo za kupambana na changamoto zinazo wazunguka. Zawadi Kwa Watanzania ni moja ya suluhisho sahihi la changamoto zako. Ni vyema kila mtanzania akapata nakala na kukisoma kitabu hiki hutakuwa kama alivyokuwa. Aidha, kwa kushiriki kuwapatia ndugu, jamaa na marafiki zawadi ya kitabu hiki, utakuwa umeshiriki katika kuelimisha jamii yetu kufikia maendeleo ya pamoja.
Hakikisha Hukosi Nakala Yako ya Hard Copy (Printed) Au Softcopy (E-Book)
Zawadi Kwa Watanzania! Twende pamoja sasa tufurahie Zawadi kwa Watanzania. Zawadi ya KWELI ni kweli.
Ni mimi Peter Mkufya,
Mkufunzi na Mhamasishaji Maendeleo,
Mwanzilishi wa Kampuni ya Must Lead Ltd.
Whatsapp namba 0786 202 202